WAZIRI WA FEDHA, DKT WILLIUM MGIMWA HATUNAYE TENA DUNIANI...

Habari zilizoufikia mtandao huu hivi punde zinasema kuwa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa amefariki dunia huko nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa katika Hospitali ya Mediclinic Kloff. 

Habari zaidi kuhusu msiba huu zitawajia kadri zitakavyokuwa zikipatikana. Mungu ilaze roho ya marehemu, Dkt. Mgimwa mahala pema , Amina.

KONDOA WILAYA KONGWE YENYE MIUNDO MBINU 'BUTU' NA MAISHA DUNI


Daraja hili halijawahi kupitisha gari kwa miaka kadhaa sasa, lakini limekuwa likijengwa karibu kila mwaka na kabomolewa na maji ya mbua...sijui kulikoni...na sijui fedha za ujenzi zinapatikana wapi! Daraja hili lipo kijiji cha Itiso barabara ya Kondoa-Bolisa.
Daraja la Kolo, Kondoa, hivi viongozi hawakuliona hilo miaka yote hiyo? Tushukuru Mwenyezi Mungu barabara hiyo sasa itajengwa kwa kiwango cha lami huenda ndio suluhisho la magari kupitia korongoni miaka yote  
Darasa la Kolo katika barabara ya Dodoma-Arusha, lilivunjika miaka zaidi ya 15 iliyopita hadi leo halijajengwa, lingekuwa na Sarenda Dar es salaam, Karanga Moshi au Nduruma Arusha ingekuweje?

WILAYA ya Kondoa mkoani Dodoma ni moja ya Wilaya kongwe nchini, inasadikiwa Iliana rasmi miaka 87 iliyopita, ikiwa ni miaka 35 kabla ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 na miaka 52 baada ya uhuru huo, yaani ilihali wa rasmi mwaka 1926.

Makao ya Makuu ya Wilaya hii inaaminika ndipo yalipokuwa Makao Makuu ya Jimbo la kanda ya Kati (Central Province) lilojumuisha Meiji mikuu ya Dodoma, Mpwapwa na Singida wakati huo,ambapo wakoloni wa Kijerumani wapokea kodi za mababu zetu mjini Kondoa pamoja na mikusanyiko na maamuzi yote ya utawala wa kikoloni ilifanyika hapo.

Jengo hili hapa chini linalosadikiwa kuwa iliojengwa mwaka 1902 na Wakoloni hao wa Kijerumani kwa nguvu za watanganyika wakati huo. Sasa jengo hilo linatumika kuwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kondoa na Ofisi zingine.




Wilaya hii licha ya ukongwe huo barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami ni kilomita tatu, tu kati ya tano zilizoahidiwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa safari zake Dkt. Jakaya Kikwete kati ya kilomita zaidi ya 800 za barabara wilayani hapa.

Lakini licha ya barabara ndefu na muhimu barani Afrika inayotoka Cape Town Afrika ya Kusini hadi Cairo Misri kupitia wilayani Kondoa na Chemba kwa zaidi ya kilomita 170 ndiyo kipande kilichobaki kirefu hakijajengwa kwa kiwango cha lami jambo linalokwamisha maendeleo ya wananchi wa eneo hili.
 

NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI SAMBAMBA NA UTORO DIDIMIZO LA ELIMU KITETO MKOANI MANYARA.



HALI ya maendeleo ya elimu wilaya ya Kiteto mkoani Manyara bado tete baada ya jamii kuendeleza kubariki ndoa za utotoni, mimba na utoro shuleni, huku siasa zikizidi kuathiri miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii kusita kuchangia maendeleo hayo.

Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA Bw. Samuel Kerinja akitoa neno la awali kabla ya Ufunguzi wa mkutano
                                           
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Kiteto na kushirikisha makundi mbalimbali wakiwemo, madiwani, Wenyeviti wa vijiji na watendaji, viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali na wawakilishi wa Halmashauri hiyo.

Hayo yalibainika juzi katika mkutano wa wadau wa maendeleo wakiwemo Madiwani, Wenyeviti wa Vijiji, Watendaji na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiseriali wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara kujadili taarifa ta utafiti wa maendeleo ya elimu na ujenzi uliofanywa na Shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Diwani kata ya Chapakazi  Lainumbe Mollel alisema wanachi wameathiriwa na siasa kwa kuwasilikiza zaidi wanasiasa badala ya kushughulikia shughuli za maendeleo, lakini pia kuchelewa kwa fedha kutoka serikali kuu ni sababu nyingine inayokwamisha mipango ya maendeleo siyo ya elimu tu bali ya Nyanja zote.
Alisema viongozi wa vitongoji na vijiji wamekuwa wakiitisha mikutano bila mafanikio wananchi hawataki kuitikia mikutano hiyo, sababu ni mipango ya maendeleo kuingiliwa na siasa, lakini pia wamekuwa wakipitisha bajeti Halmashauri za Wilaya lakini pesa hazifiki kwa wakati jambo linaloathiri mipango hiyo.
Diwani Viti maalumu   Zuhura Mavumbi alisema utafiti uliofanywa na KINNAPA umedhihirisha madhaifu makubwa katika maendeleo ya elimu wilayani Kiteto na kwamba hakuna budi kuhakikisha jamii inabadilika.
“Tafiti zinafanyika kweli lakini utafiti uliofanywa na KINNAPA umetuongezea ufahamu juu ya madhaifu tuliyonayo…watoto wetu sisi makabila ya Wanguu na Wamasai hatuna kazi nao zaidi ya kuwaozesha na kupokea mahari, maana yake ni kwamba bado Kiteto hatujapokea elimu ipasavyo kwani licha ya uhaba wa walimu na vifaa bado hali yetu ni mbaya” Alisema  Zuhura.




Afisa Miradi wa Shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA Bw. Dinno Celestian akiwasilisha mada katika mkutano huo wa wadau wa maendeleo ya Wilaya ya Kiteto

Awali Mratibu wa KINNAPA Samwel Kerinja alisema KINNAPA itaendelea kufanya tafiti na kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kijamii yanayoikabili jamii kwa jumla ili kusukuma maendeleo mbele hasa kwa jamii wafugaji na waokota matunda.
                                                      
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Nainge Lemalali akiugua mkutano wa wadau wa maendeleo wa Wilaya ya Kiteto mkoani



Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye pia ni Mwneyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Nainge Lemalali alisema hali ya Wilaya ya Kiteto kimaendeleo ni bora ukilinganisha na awali kwani imepiga hatua kubwa.
“Ni kweli hali ni mbaya lakini ukilinganisha na miaka 10 iliyopita bado tunaamini hatua kubwa tumepiga licha ya mapungufu kadhaa yaliyomo…jambo la muhimu ni kuhakikisha tunasonga mbele kwa kushirikiana na si kutupiana lawama bila kutafuta suluhisho kwa pamoja”Alisema  Lemalali.
Utafiti huo wa uwajibikaji ulifanywa na KINNAPA kwakushirikiana na Halmashauri ya Kiteto katika vijiji takribani 20 vya kata 13 kwa miaka miwili sasa wakiamini maendeleo huletwa na maarifa, ubunifu, mipango sahihi na bora, matumizi na usimamizi wa busara wa rasilimali zilizopo.


Mmoja wa wadau wa maendeleo wilayani Kiteto Bw. Fratern Kwahhison akichagia mada katika mkutano huo

M/KITI WA ZAMANI WA MONDULI DAVID PELLO AZIKWA NYUMBANI KWAKE MAKUYUNI, WAZIRI MKUU MSTAAFU BW. EDWARD LOWASSA AMWAGIA SIFA TELE TELE.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli na Diwani wa Makuyuni marehemu David Pello
                                                          
safari ya mwisho ya David Pello
                                                                           
 WAZIRI Mkuu Mstaafu Bw. Edward Lowassa amemwagia sifa aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Marehemu David Pello katika mazishi yake yaliyofanyika nyumbanai kwake Makuyuni leo.

Amesema anamjua Pello kwa mambo makuu matatu, kwanza alimsaidia sana mwaka 1993 katika maandalizi ya kugombea ubunge wa Monduli na hatimaye kunyakua  kiti hicho mwaka 1995, walipigana kufa kupona kuhakikisha kata ya Makuyuni haimegwi kwenda Mkoa wa Manyara wakati wa zoezi hilo miaka ya mwanzo ya 2000 lakini pia kuhakikisha Mji wa Makuyuni unapata maji ya uhakika.
                                                               
Mbunge wa Mondoli, Edward Lowasssa Akimsalimu mjane wa marehem
                                                          
WAZIRI Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho leo kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli na Diwani wa Makuyuni marehemu David Pello muda mfupi kabla ya mazishi yake nyumbani kwake Makuyuni, wilayani Monduli, Arusha.


"Nilipata habari nikiwa Mji wa Cape Town Afrika  ya Kusini mahali ambapo bahari za Atlantiki na Pasfiki zilipokutana nikalazimika kuondoka kuwahi kumzika ndugu yangu, ndugu yetu, lakini nasikitika kutokana na sababu zisizozuilika mke  wangu ameshindwa kufika...kubwa tuige mazuri ya David alikuwa binadamu kama sisi na hakosi makosa"Alisema kwa msisitizo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Bw. Vicent Parseko akitoa salamu alimtaja Pello kama mpiganaji mahiri katika maisha ya binadamu na kamwe hatosahaulika kwa juhudi zake katika kupigania maisha ya watu wa Makuyuni, Monduli na taifa kwa ujumla.

Mchungaji aliyeongoza mazishi hayo, Elijah Mollel alisema kifo cha Pello si huzuni kwa ndugu zake tu bali ni huzuni kwa wanadamu wote, na iwapo familia ilikuwa na mgawanyiko sasa ndio wakati wa kushirikiana pamoja kwani maisha yataendelea licha ya kutokwa na ndugu yao.

"Huu ni wakati wa mapambano baina yenu, ni wakati wa kupendana, kushikamana, kupambana kimaisha....hakuna sababu ya kuogopa kwani yatima mjane na watu wa Mungu, misiope kwani Mungu yupo na anaendelea kuwepo" alisisitiza.

Marehemu Pello alishirikilia kiti cha Udiwani kata ya Makuyuni kwa vipindi vinne na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli kwa vipindi viwili, Alizaliwa mwaka 1955  pia alikuwa Mwenyekiti wa viongozi wa Mila ya Kimasai (Laigwanani) kata ya Makuyuni hadi kifo chake. Alifariki ghafla Desemba 22 mwaka huu nyumbani kwake makuyuni.
                                                                  


Katika mazishi ya marehemu David Pello wa Makuyuni, katikati ni waziri Mstaafu na mbunge wa Monduli Edward Lowassa, kulia kwake Mwenyekiti CCM Wilya ya Monduli Reuben Kunei na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Bw.  Kasunga, kushoto kwake Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jaji Rutta na Mkuu wa Mkoa wa Singida Parseko Ole Kone
                                                      
Mh, Lowassa Akitoa neno la mwisho
                                                    
mh, Lowassa Akiaga kuondoka 
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya n

viongozi wabainishwa kuwa chanzo cha migogoro ya wakulima na wafugaji



Na Said Njuki
WAKATI migogoro ya wakulima na wafugaji ikishika kasi nchini, Mashirika yasiyo ya kiserikali  (NGO's) mkoani Manyara yamedai kukithiri kwa migogoro hiyo kunatokana  na udhaifu wa uongozi bora na uwajibikaji kwa viongozi wa serikali.

Mashirika hayo yamedai kitendo cha migogoro hiyo kuibuka kila kona ya nchi ni aibu katika nchi inayotawaliwa kwa misingi ya utawala bora wakati viongozi wa serikali wa ngazi mbalimbali wapo kila kona, lakini kila taarifa za migogoro hiyo zimekuwa zikiripotiwa kila siku jambo ambalo ni hatari.

"Inasikitisha kusikia migogoro ya wafugaji na wakulima karibu kila kona ya nchi yetu,wakati viongozi wapo...matukio hayo ambayo mengine yanaambatana na mauaji huku wengine wakijeruhiwa na kubakia na vilema vya maisha ni vielelezo wazi kuwa upo udhaifu mkubwa wa utawala bora na uwajibikaji kwa viongozi wetu". Alisema  Mratibu wa mtandao wa mashirika hayo Mkoa wa Manayara (MACSNET) Bw. Nemence  Mabung'ai.

Bw. Mabung'ai alisema hayo katika mafunzo ya siku mbili ya wanachama wa mtandao huo juu ya jinsi ya mbinu za kuandika historia za miradi yenye mafanikio yaliyofanyiji mjini Babati Manyara na kuhudhuriwa na viongozi wa mashirika hayo zaidi ya 30 kutoka Wilaya za Babati, Kiteto, Simanjiro, Hanang na Mbulu.

" Serikali ya Tanzania ilishagawa kila eneo linamilikiwa na serikali za vijiji, Wilaya, Mkoa na taifa na  kila eneo linalo viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa
...hata  hivyo bado maeneo mengi yenye viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya Kitongoji, kijiji, kata, Wilaya hadi Mkoa sheria,za ardhi zipo, lakini bado mapigano mengi  yanatokea  kwanini kama siyo uongozi mbovu na usiowajibika? " Alihoji Bw. Mabung'ai.

Alisema kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamekuwa wakipambana na hali hiyo kwa muda mrefu kwa kutoa elimu na kwamba kinachokwamisha kwa kiasi kikubwa ni viongozi hao kutowajibika ipasavyo na kwamba mifumo ya uongozi na uwajibikaji ingetekelezwa vizuri migogoro hiyo ingefikia mwisho.

Alishauri viongozi wenye maeneo yenye migogoro hiyo wakae pamoja na wadau husika kupanga kuweka mipango ya matumizi bora ya ardhi na kusimamia mipaka hiyo, tofauti na hilo migogoro haitaosha nchii.

Kiongozi wa Shirika lisilo la kiserikali la  Hanang Wemen Concelling Development  Association (HAOCODA) Bi. Rose Tippe alisema tatizo ni utendaji mbovu kwa wasimamizi wa sheria, lakini bado mashirika hao yanafanya kazi kubwa ya na yanastahiki pongezi kwa jitihada zao katika kupigania haki za wafugaji na wakulima hao



WANAFUNZI 48 WA SHULE YA KIISLAM YA CHAMANZI WAHITIM MAFUNZO YA SKAUTI


baadhi ya skauti wakitoka katika uchunguzi wa shughuli  za kijamii katika tasisi mbalimbali kama polisi , sokoni, n.k, kama sehem ya mafunzo yao
skauti wakisikiliza maelezo ya mkufunzi wao baada ya kutoka katika shughuli za kijamii
Na Said Njuki Dar es Salaam

SKAUTI 48 wa Shule ya Msingi ya Kiislamu ya Chamazi wamepata mafunzo ya kijasiri kwa lengo la kuwajenga kikakamavu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kujitegemea kimaisha.

"Malengo hasa ni  kumwandaa vijana w awe wakakamavu, jasiri waweze  kujitegemea na hatimaye wawe ni msaada kwa jamii ikiwa ni pamoja na kujiandaa kiakili kiutafiti kwa faida ya yake, na taifa". Alisema Alhaj Omari Mavura Kamisha Msaidizi Skauti Makao Makuu.

Mavura alisema hiyo ni kambi ya Kwanza ya aina yake, ambapo wasichana 27 na wa vulana 21 na ilikuwa  ya siku nne ambapo vijana hao wenye umri kati ya miaka saba na 12 waliweza kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulinzi wa maeneo yao.

Naye mkufunzi wa mafunzo hayo Bw. Mustafa Musoma alisema kwa kawaida mafunzo hayo  hufanyika mara nne kwa mwaka ambapo mwezi wa  Desemba mwaka huu yatafanyika tena ili kwenda sambamba na mtazamo wa Shule wa kuwaandaa vijana kikakamavu.

Mkuu wa Shule hiyo Bw. Abdallah Ngorini alisema viongozi wa Shule hiyo hufarijika sana hasa vijana wanapofnya mazoezi kama hayo ni kujiweka vizuri kiafya na kiakili.

Wakufunzi wengine ni Dotto Mohamed na Abdulrahim Nassoro wa Markaz Gongolamboto.
tunakunywa chai baada ya kutoka katika mafunzo na shughuli hizo.


MWANAMKE WA BABATI ALIYEKUFA KIFO TATA KATIKA SAKATA LA OPERESHENI TOKOMEZA UJANGILI AZIKWA WIKI 3 BAADA YA KIFO CHAKE CHA KIKATILI

mwili wa marehemu Emiliana anaedaiwa kuuawa na askari wa hifadhi ya TANAPA ukiwa kanisani katika ibada maalum ya kumuombea Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi
Na Said Njuki Babati


MWANAMKE  Emiliana Maro (42) aliyekuwa  kifo cha utata baada ya kuchukuliwa na timu ya Operesheni Tokomeza Ujangili wiki tatu zilizopita amezikwa juzi Jumamosi kijiji cha Oringadida  kata ya Qash Wilaya ya Babati mkoani Manyara.

Katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa watu kutoka pembe zote za Wilaya ya Babati na nje ya Wilaya hiyo,  hakuna kiongozi wa serikali wa ngazi ya Wilaya na Mkoa aliyehudhuria mbali na viongozi wa vyama vya Siasa  akiwemo mbunge wa Babati vijijini Bw. Jitu Soni  (CCM), Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wolaya ya Babati vijijini Bw. Nicodemus Tarimo huku  CHADEMA wakitumia  wawakilishi.
Baadhi ya wanafamilia wa marehem Emiliana Kibuga wakihuzunika kwa kifo tata cha ndugu yao inayodaiwa kusababishwa na askari wa Tarangire
Inadaiwa marehemu  Emiliana alichukuliwa na timu hiyo Oktoba 16 asubuhi ambapo jioni alirudishwa na askari hao akiwa taabani kwa ajili ya upekuzi  huku watoto wake Shaabani na Morgan wakiwa kwenye ulinzi mkali na kisha kuondoka naye tena hadi walipopiqiwa simu na Polisi wakitakiwa kuchukua mwili wa mtuhumiwa huyo.
mmoja wa watoto wa marehem Emiliana Kibuga akiuaga mwili wa mama yake mzazi
Awali, kabla ya mazishi hayo pikipiki zaidi ya 200 na gari 70 za Kata hizo zilisitisha kazi kwa ajili ya kwenda kuchukua na kuusindiki-mwili wa marehemu toka mochwari ya hospitali ya Mrara mjini Babati hadi nyumbani, huku wasindikizaji hao wakiwa na mapango yenye ujumla mbalimbali.

Baadhi tu yaliandikwa ' Lini mwanamke akauwa tembo? Paki (TANAPA) marufuku kukanyaga Galapo na mwaka 2015 tembo waende kupiga kura'
huku wakilaani waliohusika na mauaji hayo.

Paroko wa Kanisa Katoliki Galapo Baba Eugene Kubasu akiongoza Ibada aliitaka serikali kuhakikisha waliofanya unyama huo wanabainika na kuchukuliwa hatua za kisheria na wao na wananchi kwa ujumla wapiga magoti wakimshitakia Mwenyezi Mungu haki itendeke na si vinginevyo.

Mwakilishi wa Kamati ya mazishi Bw. Jumanne Mwanja akisoma wasifu wa marehemu kwa niaba ya familia alisema kwa mujibu wa mume wa marehemu huyo Bw. Elias Kibuga mke wake hakuwa na magonjwa ng'ang'anizi kama shinikizo la damu, sukari au vidonda vya tumbo, amekuwa akiugua magonjwa yenye kutibika kwa urahisi.

Pia familia hiyo ilieleza kuwa kitendo kilichofanywa na timu ya Oporesheni Tokomeza Ujangili dhidi ya mwanamke huyo na wengine nchini katika kipindi hicho ni ukiukaji wa sheria za nchi hivyo kuiomba serikali kuchukua hatua wahusika bila kuwaonea haya.
Mbunge wa jimbo hilo bwana Jitu akiweka shada la maua katika kaburi la Emiliana Kibuga anaedaiwa kuuawa na askari wa Tarangire
Mbunge wa Babati vijijini Bw. Jitu alisema tukio hilo limewasikitisha sana kama wabunge na kuahidi kwamba wabunge wote wa Mkoa wa Manyara watahakikisha sheria inashika mkondo wake.

Hata hivyo licha ya umma kufurika kuuaga mwili huo huku wengi wao wakitamani kushuhudia uso wa marehemu, familia ilikataa kata kata kuweka uso wazi kwa madai ya sababu maalumu.
mume wa marehemu Emiliana Kibuga akiuaga mwili wa mkewe  huku akinyanyua hadi picha hiyo kwa huzuni kubwa baada ya kuachiwa ambaye nae alitekwa kabla ya mkewe na askari hao lakini baadae kuachiwa baada ya mkewe kuuawa
Add caption
Wananchi kwa uapnde wao walilazimisha kufunguliwa kwa mwili huo, hadi Kiongozi wa Kamati ya mazishi na musemaji wa familia Bw. Godwin Sanda alipowasihi wananchi hao kukubaliana na uamuzi huo.
majirani, ndugu jamaa na marafiki wa familia ya Emiliana kibuga wakiuaga mwili wa mpendwa wao



hatimaye mwili wa Emiliana umezikwa,

NJUKI BLOG INAWAPA POLE  WOTE WALIOGUSWA NA MSIBA HUO
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEM EMILIANA MAHALA PEMA PEPONI
AMINA

Older Posts