M/KITI WA ZAMANI WA MONDULI DAVID PELLO AZIKWA NYUMBANI KWAKE MAKUYUNI, WAZIRI MKUU MSTAAFU BW. EDWARD LOWASSA AMWAGIA SIFA TELE TELE.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli na Diwani wa Makuyuni marehemu David Pello
                                                          
safari ya mwisho ya David Pello
                                                                           
 WAZIRI Mkuu Mstaafu Bw. Edward Lowassa amemwagia sifa aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Marehemu David Pello katika mazishi yake yaliyofanyika nyumbanai kwake Makuyuni leo.

Amesema anamjua Pello kwa mambo makuu matatu, kwanza alimsaidia sana mwaka 1993 katika maandalizi ya kugombea ubunge wa Monduli na hatimaye kunyakua  kiti hicho mwaka 1995, walipigana kufa kupona kuhakikisha kata ya Makuyuni haimegwi kwenda Mkoa wa Manyara wakati wa zoezi hilo miaka ya mwanzo ya 2000 lakini pia kuhakikisha Mji wa Makuyuni unapata maji ya uhakika.
                                                               
Mbunge wa Mondoli, Edward Lowasssa Akimsalimu mjane wa marehem
                                                          
WAZIRI Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho leo kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli na Diwani wa Makuyuni marehemu David Pello muda mfupi kabla ya mazishi yake nyumbani kwake Makuyuni, wilayani Monduli, Arusha.


"Nilipata habari nikiwa Mji wa Cape Town Afrika  ya Kusini mahali ambapo bahari za Atlantiki na Pasfiki zilipokutana nikalazimika kuondoka kuwahi kumzika ndugu yangu, ndugu yetu, lakini nasikitika kutokana na sababu zisizozuilika mke  wangu ameshindwa kufika...kubwa tuige mazuri ya David alikuwa binadamu kama sisi na hakosi makosa"Alisema kwa msisitizo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Bw. Vicent Parseko akitoa salamu alimtaja Pello kama mpiganaji mahiri katika maisha ya binadamu na kamwe hatosahaulika kwa juhudi zake katika kupigania maisha ya watu wa Makuyuni, Monduli na taifa kwa ujumla.

Mchungaji aliyeongoza mazishi hayo, Elijah Mollel alisema kifo cha Pello si huzuni kwa ndugu zake tu bali ni huzuni kwa wanadamu wote, na iwapo familia ilikuwa na mgawanyiko sasa ndio wakati wa kushirikiana pamoja kwani maisha yataendelea licha ya kutokwa na ndugu yao.

"Huu ni wakati wa mapambano baina yenu, ni wakati wa kupendana, kushikamana, kupambana kimaisha....hakuna sababu ya kuogopa kwani yatima mjane na watu wa Mungu, misiope kwani Mungu yupo na anaendelea kuwepo" alisisitiza.

Marehemu Pello alishirikilia kiti cha Udiwani kata ya Makuyuni kwa vipindi vinne na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli kwa vipindi viwili, Alizaliwa mwaka 1955  pia alikuwa Mwenyekiti wa viongozi wa Mila ya Kimasai (Laigwanani) kata ya Makuyuni hadi kifo chake. Alifariki ghafla Desemba 22 mwaka huu nyumbani kwake makuyuni.
                                                                  


Katika mazishi ya marehemu David Pello wa Makuyuni, katikati ni waziri Mstaafu na mbunge wa Monduli Edward Lowassa, kulia kwake Mwenyekiti CCM Wilya ya Monduli Reuben Kunei na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Bw.  Kasunga, kushoto kwake Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jaji Rutta na Mkuu wa Mkoa wa Singida Parseko Ole Kone
                                                      
Mh, Lowassa Akitoa neno la mwisho
                                                    
mh, Lowassa Akiaga kuondoka 
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya n

Newer Post Older Post

Leave a Reply