MWANAMKE WA BABATI ALIYEKUFA KIFO TATA KATIKA SAKATA LA OPERESHENI TOKOMEZA UJANGILI AZIKWA WIKI 3 BAADA YA KIFO CHAKE CHA KIKATILI

mwili wa marehemu Emiliana anaedaiwa kuuawa na askari wa hifadhi ya TANAPA ukiwa kanisani katika ibada maalum ya kumuombea Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi
Na Said Njuki Babati


MWANAMKE  Emiliana Maro (42) aliyekuwa  kifo cha utata baada ya kuchukuliwa na timu ya Operesheni Tokomeza Ujangili wiki tatu zilizopita amezikwa juzi Jumamosi kijiji cha Oringadida  kata ya Qash Wilaya ya Babati mkoani Manyara.

Katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa watu kutoka pembe zote za Wilaya ya Babati na nje ya Wilaya hiyo,  hakuna kiongozi wa serikali wa ngazi ya Wilaya na Mkoa aliyehudhuria mbali na viongozi wa vyama vya Siasa  akiwemo mbunge wa Babati vijijini Bw. Jitu Soni  (CCM), Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wolaya ya Babati vijijini Bw. Nicodemus Tarimo huku  CHADEMA wakitumia  wawakilishi.
Baadhi ya wanafamilia wa marehem Emiliana Kibuga wakihuzunika kwa kifo tata cha ndugu yao inayodaiwa kusababishwa na askari wa Tarangire
Inadaiwa marehemu  Emiliana alichukuliwa na timu hiyo Oktoba 16 asubuhi ambapo jioni alirudishwa na askari hao akiwa taabani kwa ajili ya upekuzi  huku watoto wake Shaabani na Morgan wakiwa kwenye ulinzi mkali na kisha kuondoka naye tena hadi walipopiqiwa simu na Polisi wakitakiwa kuchukua mwili wa mtuhumiwa huyo.
mmoja wa watoto wa marehem Emiliana Kibuga akiuaga mwili wa mama yake mzazi
Awali, kabla ya mazishi hayo pikipiki zaidi ya 200 na gari 70 za Kata hizo zilisitisha kazi kwa ajili ya kwenda kuchukua na kuusindiki-mwili wa marehemu toka mochwari ya hospitali ya Mrara mjini Babati hadi nyumbani, huku wasindikizaji hao wakiwa na mapango yenye ujumla mbalimbali.

Baadhi tu yaliandikwa ' Lini mwanamke akauwa tembo? Paki (TANAPA) marufuku kukanyaga Galapo na mwaka 2015 tembo waende kupiga kura'
huku wakilaani waliohusika na mauaji hayo.

Paroko wa Kanisa Katoliki Galapo Baba Eugene Kubasu akiongoza Ibada aliitaka serikali kuhakikisha waliofanya unyama huo wanabainika na kuchukuliwa hatua za kisheria na wao na wananchi kwa ujumla wapiga magoti wakimshitakia Mwenyezi Mungu haki itendeke na si vinginevyo.

Mwakilishi wa Kamati ya mazishi Bw. Jumanne Mwanja akisoma wasifu wa marehemu kwa niaba ya familia alisema kwa mujibu wa mume wa marehemu huyo Bw. Elias Kibuga mke wake hakuwa na magonjwa ng'ang'anizi kama shinikizo la damu, sukari au vidonda vya tumbo, amekuwa akiugua magonjwa yenye kutibika kwa urahisi.

Pia familia hiyo ilieleza kuwa kitendo kilichofanywa na timu ya Oporesheni Tokomeza Ujangili dhidi ya mwanamke huyo na wengine nchini katika kipindi hicho ni ukiukaji wa sheria za nchi hivyo kuiomba serikali kuchukua hatua wahusika bila kuwaonea haya.
Mbunge wa jimbo hilo bwana Jitu akiweka shada la maua katika kaburi la Emiliana Kibuga anaedaiwa kuuawa na askari wa Tarangire
Mbunge wa Babati vijijini Bw. Jitu alisema tukio hilo limewasikitisha sana kama wabunge na kuahidi kwamba wabunge wote wa Mkoa wa Manyara watahakikisha sheria inashika mkondo wake.

Hata hivyo licha ya umma kufurika kuuaga mwili huo huku wengi wao wakitamani kushuhudia uso wa marehemu, familia ilikataa kata kata kuweka uso wazi kwa madai ya sababu maalumu.
mume wa marehemu Emiliana Kibuga akiuaga mwili wa mkewe  huku akinyanyua hadi picha hiyo kwa huzuni kubwa baada ya kuachiwa ambaye nae alitekwa kabla ya mkewe na askari hao lakini baadae kuachiwa baada ya mkewe kuuawa
Add caption
Wananchi kwa uapnde wao walilazimisha kufunguliwa kwa mwili huo, hadi Kiongozi wa Kamati ya mazishi na musemaji wa familia Bw. Godwin Sanda alipowasihi wananchi hao kukubaliana na uamuzi huo.
majirani, ndugu jamaa na marafiki wa familia ya Emiliana kibuga wakiuaga mwili wa mpendwa wao



hatimaye mwili wa Emiliana umezikwa,

NJUKI BLOG INAWAPA POLE  WOTE WALIOGUSWA NA MSIBA HUO
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEM EMILIANA MAHALA PEMA PEPONI
AMINA

Newer Post Older Post

Leave a Reply