viongozi wabainishwa kuwa chanzo cha migogoro ya wakulima na wafugaji



Na Said Njuki
WAKATI migogoro ya wakulima na wafugaji ikishika kasi nchini, Mashirika yasiyo ya kiserikali  (NGO's) mkoani Manyara yamedai kukithiri kwa migogoro hiyo kunatokana  na udhaifu wa uongozi bora na uwajibikaji kwa viongozi wa serikali.

Mashirika hayo yamedai kitendo cha migogoro hiyo kuibuka kila kona ya nchi ni aibu katika nchi inayotawaliwa kwa misingi ya utawala bora wakati viongozi wa serikali wa ngazi mbalimbali wapo kila kona, lakini kila taarifa za migogoro hiyo zimekuwa zikiripotiwa kila siku jambo ambalo ni hatari.

"Inasikitisha kusikia migogoro ya wafugaji na wakulima karibu kila kona ya nchi yetu,wakati viongozi wapo...matukio hayo ambayo mengine yanaambatana na mauaji huku wengine wakijeruhiwa na kubakia na vilema vya maisha ni vielelezo wazi kuwa upo udhaifu mkubwa wa utawala bora na uwajibikaji kwa viongozi wetu". Alisema  Mratibu wa mtandao wa mashirika hayo Mkoa wa Manayara (MACSNET) Bw. Nemence  Mabung'ai.

Bw. Mabung'ai alisema hayo katika mafunzo ya siku mbili ya wanachama wa mtandao huo juu ya jinsi ya mbinu za kuandika historia za miradi yenye mafanikio yaliyofanyiji mjini Babati Manyara na kuhudhuriwa na viongozi wa mashirika hayo zaidi ya 30 kutoka Wilaya za Babati, Kiteto, Simanjiro, Hanang na Mbulu.

" Serikali ya Tanzania ilishagawa kila eneo linamilikiwa na serikali za vijiji, Wilaya, Mkoa na taifa na  kila eneo linalo viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa
...hata  hivyo bado maeneo mengi yenye viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya Kitongoji, kijiji, kata, Wilaya hadi Mkoa sheria,za ardhi zipo, lakini bado mapigano mengi  yanatokea  kwanini kama siyo uongozi mbovu na usiowajibika? " Alihoji Bw. Mabung'ai.

Alisema kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamekuwa wakipambana na hali hiyo kwa muda mrefu kwa kutoa elimu na kwamba kinachokwamisha kwa kiasi kikubwa ni viongozi hao kutowajibika ipasavyo na kwamba mifumo ya uongozi na uwajibikaji ingetekelezwa vizuri migogoro hiyo ingefikia mwisho.

Alishauri viongozi wenye maeneo yenye migogoro hiyo wakae pamoja na wadau husika kupanga kuweka mipango ya matumizi bora ya ardhi na kusimamia mipaka hiyo, tofauti na hilo migogoro haitaosha nchii.

Kiongozi wa Shirika lisilo la kiserikali la  Hanang Wemen Concelling Development  Association (HAOCODA) Bi. Rose Tippe alisema tatizo ni utendaji mbovu kwa wasimamizi wa sheria, lakini bado mashirika hao yanafanya kazi kubwa ya na yanastahiki pongezi kwa jitihada zao katika kupigania haki za wafugaji na wakulima hao



Newer Post Older Post

Leave a Reply