NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI SAMBAMBA NA UTORO DIDIMIZO LA ELIMU KITETO MKOANI MANYARA.



HALI ya maendeleo ya elimu wilaya ya Kiteto mkoani Manyara bado tete baada ya jamii kuendeleza kubariki ndoa za utotoni, mimba na utoro shuleni, huku siasa zikizidi kuathiri miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii kusita kuchangia maendeleo hayo.

Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA Bw. Samuel Kerinja akitoa neno la awali kabla ya Ufunguzi wa mkutano
                                           
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Kiteto na kushirikisha makundi mbalimbali wakiwemo, madiwani, Wenyeviti wa vijiji na watendaji, viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali na wawakilishi wa Halmashauri hiyo.

Hayo yalibainika juzi katika mkutano wa wadau wa maendeleo wakiwemo Madiwani, Wenyeviti wa Vijiji, Watendaji na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiseriali wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara kujadili taarifa ta utafiti wa maendeleo ya elimu na ujenzi uliofanywa na Shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Diwani kata ya Chapakazi  Lainumbe Mollel alisema wanachi wameathiriwa na siasa kwa kuwasilikiza zaidi wanasiasa badala ya kushughulikia shughuli za maendeleo, lakini pia kuchelewa kwa fedha kutoka serikali kuu ni sababu nyingine inayokwamisha mipango ya maendeleo siyo ya elimu tu bali ya Nyanja zote.
Alisema viongozi wa vitongoji na vijiji wamekuwa wakiitisha mikutano bila mafanikio wananchi hawataki kuitikia mikutano hiyo, sababu ni mipango ya maendeleo kuingiliwa na siasa, lakini pia wamekuwa wakipitisha bajeti Halmashauri za Wilaya lakini pesa hazifiki kwa wakati jambo linaloathiri mipango hiyo.
Diwani Viti maalumu   Zuhura Mavumbi alisema utafiti uliofanywa na KINNAPA umedhihirisha madhaifu makubwa katika maendeleo ya elimu wilayani Kiteto na kwamba hakuna budi kuhakikisha jamii inabadilika.
“Tafiti zinafanyika kweli lakini utafiti uliofanywa na KINNAPA umetuongezea ufahamu juu ya madhaifu tuliyonayo…watoto wetu sisi makabila ya Wanguu na Wamasai hatuna kazi nao zaidi ya kuwaozesha na kupokea mahari, maana yake ni kwamba bado Kiteto hatujapokea elimu ipasavyo kwani licha ya uhaba wa walimu na vifaa bado hali yetu ni mbaya” Alisema  Zuhura.




Afisa Miradi wa Shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA Bw. Dinno Celestian akiwasilisha mada katika mkutano huo wa wadau wa maendeleo ya Wilaya ya Kiteto

Awali Mratibu wa KINNAPA Samwel Kerinja alisema KINNAPA itaendelea kufanya tafiti na kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kijamii yanayoikabili jamii kwa jumla ili kusukuma maendeleo mbele hasa kwa jamii wafugaji na waokota matunda.
                                                      
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Nainge Lemalali akiugua mkutano wa wadau wa maendeleo wa Wilaya ya Kiteto mkoani



Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye pia ni Mwneyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Nainge Lemalali alisema hali ya Wilaya ya Kiteto kimaendeleo ni bora ukilinganisha na awali kwani imepiga hatua kubwa.
“Ni kweli hali ni mbaya lakini ukilinganisha na miaka 10 iliyopita bado tunaamini hatua kubwa tumepiga licha ya mapungufu kadhaa yaliyomo…jambo la muhimu ni kuhakikisha tunasonga mbele kwa kushirikiana na si kutupiana lawama bila kutafuta suluhisho kwa pamoja”Alisema  Lemalali.
Utafiti huo wa uwajibikaji ulifanywa na KINNAPA kwakushirikiana na Halmashauri ya Kiteto katika vijiji takribani 20 vya kata 13 kwa miaka miwili sasa wakiamini maendeleo huletwa na maarifa, ubunifu, mipango sahihi na bora, matumizi na usimamizi wa busara wa rasilimali zilizopo.


Mmoja wa wadau wa maendeleo wilayani Kiteto Bw. Fratern Kwahhison akichagia mada katika mkutano huo

Newer Post Older Post

Leave a Reply