HALI ya maendeleo ya elimu wilaya ya Kiteto
mkoani Manyara bado tete baada ya jamii kuendeleza kubariki ndoa za utotoni,
mimba na utoro shuleni, huku siasa zikizidi kuathiri miradi mbalimbali ya
maendeleo kwa jamii kusita kuchangia maendeleo hayo.
|
Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA Bw.
Samuel Kerinja akitoa neno la awali kabla ya Ufunguzi wa mkutano
|
|
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo uliofanyika
ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Kiteto na kushirikisha makundi mbalimbali
wakiwemo, madiwani, Wenyeviti wa vijiji na watendaji, viongozi wa mashirika
yasiyo ya kiserikali na wawakilishi wa Halmashauri hiyo.
Hayo yalibainika juzi katika mkutano wa wadau
wa maendeleo wakiwemo Madiwani, Wenyeviti wa Vijiji, Watendaji na wawakilishi
wa mashirika yasiyo ya kiseriali wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara kujadili
taarifa ta utafiti wa maendeleo ya elimu na ujenzi uliofanywa na Shirika lisilo
la kiserikali la KINNAPA kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Diwani kata ya Chapakazi Lainumbe
Mollel alisema wanachi wameathiriwa na siasa kwa kuwasilikiza zaidi wanasiasa
badala ya kushughulikia shughuli za maendeleo, lakini pia kuchelewa kwa fedha
kutoka serikali kuu ni sababu nyingine inayokwamisha mipango ya maendeleo siyo
ya elimu tu bali ya Nyanja zote.
Alisema viongozi wa vitongoji na vijiji
wamekuwa wakiitisha mikutano bila mafanikio wananchi hawataki kuitikia mikutano
hiyo, sababu ni mipango ya maendeleo kuingiliwa na siasa, lakini pia wamekuwa
wakipitisha bajeti Halmashauri za Wilaya lakini pesa hazifiki kwa wakati jambo
linaloathiri mipango hiyo.
Diwani Viti maalumu Zuhura
Mavumbi alisema utafiti uliofanywa na KINNAPA umedhihirisha madhaifu makubwa
katika maendeleo ya elimu wilayani Kiteto na kwamba hakuna budi kuhakikisha
jamii inabadilika.
“Tafiti zinafanyika kweli lakini utafiti
uliofanywa na KINNAPA umetuongezea ufahamu juu ya madhaifu tuliyonayo…watoto
wetu sisi makabila ya Wanguu na Wamasai hatuna kazi nao zaidi ya kuwaozesha na
kupokea mahari, maana yake ni kwamba bado Kiteto hatujapokea elimu ipasavyo
kwani licha ya uhaba wa walimu na vifaa bado hali yetu ni mbaya” Alisema
Zuhura.
|
Afisa Miradi wa Shirika lisilo la
kiserikali la KINNAPA Bw. Dinno Celestian akiwasilisha mada katika mkutano huo
wa wadau wa maendeleo ya Wilaya ya Kiteto
Awali Mratibu wa KINNAPA Samwel Kerinja
alisema KINNAPA itaendelea kufanya tafiti na kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya
kijamii yanayoikabili jamii kwa jumla ili kusukuma maendeleo mbele hasa kwa
jamii wafugaji na waokota matunda.
|
|
|
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
Bw. Nainge Lemalali akiugua mkutano wa wadau wa maendeleo wa Wilaya ya Kiteto
mkoani |
Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye pia ni
Mwneyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Nainge Lemalali alisema hali
ya Wilaya ya Kiteto kimaendeleo ni bora ukilinganisha na awali kwani imepiga
hatua kubwa.
“Ni kweli hali ni mbaya lakini ukilinganisha
na miaka 10 iliyopita bado tunaamini hatua kubwa tumepiga licha ya mapungufu
kadhaa yaliyomo…jambo la muhimu ni kuhakikisha tunasonga mbele kwa kushirikiana
na si kutupiana lawama bila kutafuta suluhisho kwa pamoja”Alisema
Lemalali.
Utafiti huo wa uwajibikaji ulifanywa na
KINNAPA kwakushirikiana na Halmashauri ya Kiteto katika vijiji takribani 20 vya
kata 13 kwa miaka miwili sasa wakiamini maendeleo huletwa na maarifa, ubunifu,
mipango sahihi na bora, matumizi na usimamizi wa busara wa rasilimali zilizopo.
|
Mmoja wa wadau wa maendeleo
wilayani Kiteto Bw. Fratern Kwahhison akichagia mada katika mkutano huo
|