M/KITI WA ZAMANI WA MONDULI DAVID PELLO AZIKWA NYUMBANI KWAKE MAKUYUNI, WAZIRI MKUU MSTAAFU BW. EDWARD LOWASSA AMWAGIA SIFA TELE TELE.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli na Diwani wa Makuyuni marehemu David Pello |
safari ya mwisho ya David Pello |
WAZIRI Mkuu Mstaafu Bw. Edward Lowassa amemwagia sifa aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Marehemu David Pello katika mazishi yake yaliyofanyika nyumbanai kwake Makuyuni leo.
Amesema anamjua Pello kwa mambo makuu matatu, kwanza alimsaidia sana mwaka 1993 katika maandalizi ya kugombea ubunge wa Monduli na hatimaye kunyakua kiti hicho mwaka 1995, walipigana kufa kupona kuhakikisha kata ya Makuyuni haimegwi kwenda Mkoa wa Manyara wakati wa zoezi hilo miaka ya mwanzo ya 2000 lakini pia kuhakikisha Mji wa Makuyuni unapata maji ya uhakika.
Mbunge wa Mondoli, Edward Lowasssa Akimsalimu mjane wa marehem |
"Nilipata habari nikiwa Mji wa Cape Town Afrika ya Kusini mahali ambapo bahari za Atlantiki na Pasfiki zilipokutana nikalazimika kuondoka kuwahi kumzika ndugu yangu, ndugu yetu, lakini nasikitika kutokana na sababu zisizozuilika mke wangu ameshindwa kufika...kubwa tuige mazuri ya David alikuwa binadamu kama sisi na hakosi makosa"Alisema kwa msisitizo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Bw. Vicent Parseko akitoa salamu alimtaja Pello kama mpiganaji mahiri katika maisha ya binadamu na kamwe hatosahaulika kwa juhudi zake katika kupigania maisha ya watu wa Makuyuni, Monduli na taifa kwa ujumla.
Mchungaji aliyeongoza mazishi hayo, Elijah Mollel alisema kifo cha Pello si huzuni kwa ndugu zake tu bali ni huzuni kwa wanadamu wote, na iwapo familia ilikuwa na mgawanyiko sasa ndio wakati wa kushirikiana pamoja kwani maisha yataendelea licha ya kutokwa na ndugu yao.
"Huu ni wakati wa mapambano baina yenu, ni wakati wa kupendana, kushikamana, kupambana kimaisha....hakuna sababu ya kuogopa kwani yatima mjane na watu wa Mungu, misiope kwani Mungu yupo na anaendelea kuwepo" alisisitiza.
Marehemu Pello alishirikilia kiti cha Udiwani kata ya Makuyuni kwa vipindi vinne na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli kwa vipindi viwili, Alizaliwa mwaka 1955 pia alikuwa Mwenyekiti wa viongozi wa Mila ya Kimasai (Laigwanani) kata ya Makuyuni hadi kifo chake. Alifariki ghafla Desemba 22 mwaka huu nyumbani kwake makuyuni.
Mh, Lowassa Akitoa neno la mwisho |
mh, Lowassa Akiaga kuondoka |