KONDOA WILAYA KONGWE YENYE MIUNDO MBINU 'BUTU' NA MAISHA DUNI
Monday, 30 December 2013
Unknown
|
Daraja hili halijawahi kupitisha gari kwa miaka kadhaa sasa,
lakini limekuwa likijengwa karibu kila mwaka na kabomolewa na maji ya
mbua...sijui kulikoni...na sijui fedha za ujenzi zinapatikana wapi! Daraja hili
lipo kijiji cha Itiso barabara ya Kondoa-Bolisa.
|
|
Daraja la Kolo, Kondoa, hivi viongozi
hawakuliona hilo
miaka yote hiyo? Tushukuru Mwenyezi Mungu barabara hiyo sasa itajengwa kwa
kiwango cha lami huenda ndio suluhisho la magari kupitia korongoni miaka yote | |
|
Darasa la Kolo katika barabara ya Dodoma-Arusha,
lilivunjika miaka zaidi ya 15 iliyopita hadi leo halijajengwa, lingekuwa na
Sarenda Dar es salaam,
Karanga Moshi au Nduruma Arusha ingekuweje?
WILAYA ya Kondoa mkoani Dodoma ni moja ya Wilaya
kongwe nchini, inasadikiwa Iliana rasmi miaka 87 iliyopita, ikiwa ni miaka 35
kabla ya Uhuru wa Tanganyika
mwaka 1961 na miaka 52 baada ya uhuru huo, yaani ilihali wa rasmi mwaka 1926.
Makao ya Makuu ya Wilaya hii inaaminika ndipo yalipokuwa Makao Makuu ya Jimbo
la kanda ya Kati (Central Province) lilojumuisha Meiji mikuu ya Dodoma, Mpwapwa na
Singida wakati huo,ambapo wakoloni wa Kijerumani wapokea kodi za mababu zetu
mjini Kondoa pamoja na mikusanyiko na maamuzi yote ya utawala wa kikoloni
ilifanyika hapo.
Jengo hili hapa chini linalosadikiwa kuwa iliojengwa mwaka 1902 na Wakoloni hao
wa Kijerumani kwa nguvu za watanganyika wakati huo. Sasa jengo hilo linatumika kuwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
ya Kondoa na Ofisi zingine.
Wilaya hii licha ya ukongwe huo barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami ni
kilomita tatu, tu kati ya tano zilizoahidiwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania
wakati wa safari zake Dkt. Jakaya Kikwete kati ya kilomita zaidi ya 800 za
barabara wilayani hapa.
Lakini licha ya barabara ndefu na muhimu barani Afrika inayotoka Cape Town
Afrika ya Kusini hadi Cairo Misri kupitia wilayani Kondoa na Chemba kwa zaidi
ya kilomita 170 ndiyo kipande kilichobaki kirefu hakijajengwa kwa kiwango cha
lami jambo linalokwamisha maendeleo ya wananchi wa eneo hili. | |