mahafali ya 5 ya shule ya sekondary Chamanzi
Na Said
Njuki Dar es Salaam
MHADHIRI wa
Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro (MUM) Bw. Bilali Majuva amewataka Walimu
wa Shule nchini kubuni njia mbadala za kusomesha wanafunzi na kuacha kuwabebesha lawama wanafunzi hao
kuwa hawasomesheki.
wanafunzi wakisoma risala |
Amesema kila
mtoto anao uwezo wa kuelewa atakachosomeshwa na Mwalimu wake ipasavyo, bali
baadhi ya walimu wamekuwa wakiwatuhumu wanafunzi kuwa hawasomesheki jambo
ambalo si kweli.
"Hakuna
mwanafunzi asiyefundishika duniani, yapo malalamiko toka kwa baadhi ya walimu
kuwa baadhi ya wanafunzi hawasomesheni jambo ambalo si kweli...huko ni kukwepa
majukumu...wazazi wamewaletea watoto, wakawaamini mnaweza kuwapa elimu na
maadili mema, hawataki tena kusikia wanafunzi hawasomesheki, fundisheni watoto
wanaweza acheni kuwabebesha lawama" Alisema Bw. Majuva.
Wahitimu wavulana wa Shule ya Sekondari ya Chamazi Islamic Schools katika maafali ya 5 ya Shule hiyo yaiyofanyika Jumapili Oktoba 20 mwaka huu shuleni hapo. |
Bw. Majuva
alitoka rai hiyo Jumapili hii katika maafali ya 5 ya kidato cha IV ya Shule ya
Sekondari ya Chamazi Islamic Seminary yaliyofanyika shuleni hapo ambapo
wanafunzi zaidi ya 40 walihitimu.
Akizugumza
katika maafali hayo mgeni rasmi Bw. Issa Omari 'Malicela' ambaye pia ni
Mahadhiri katika Chuo hicho aliitaka Jamii kuelewa kuwa elimu ndiyo msingi wa
maendelo yoyote duniani.
Alisema
kitendo cha kudharau elimu yoyote ni kichocheo cha kazama katika lindi la
umaskini duniani, hivyo kukwamisha jitihada za serikali na wadau wa maendeleo
katika mapambano dhidi ya umaskini.
Awali Mkuu
wa Shule hiyo Bw. Yusuf Kokole alitoa changamoto kadhaa zinazoikabili Shule
ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maabara kwa ajili ya masons ya Kemia, Fizikia na
baiolojia, maktaba, Bwalo kwa ajili ya chakula, msikiti na kubainisha kuwa
tatizo kubwa ni uwezo mdogo wa kiuchumi.
Shule ya
chamazi Islamic seminary ipo kijiji cha Chamazi Mbagala wilayani Temeke Dar es
Salaam inayo wanafunzi kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha VI ni mekuwa
ikfanya vizuri.
Kikundi cha Skauti cha Chamazi Islamic Islamic Schools kikifanya mambo yake Jumapili Oktoba 20 mwaka huu katika maafali ya 5 ya IV Mwaka huu |
baadhi ya wageni waalikwa |