MWANAMKE WA BABATI ALIYEKUFA KIFO TATA KATIKA SAKATA LA OPERESHENI TOKOMEZA UJANGILI AZIKWA WIKI 3 BAADA YA KIFO CHAKE CHA KIKATILI
mwili wa marehemu Emiliana anaedaiwa kuuawa na askari wa hifadhi ya TANAPA ukiwa kanisani katika ibada maalum ya kumuombea Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi |
Na Said Njuki Babati
MWANAMKE Emiliana Maro (42) aliyekuwa kifo cha utata baada ya
kuchukuliwa na timu ya Operesheni Tokomeza Ujangili wiki tatu zilizopita
amezikwa juzi Jumamosi kijiji cha Oringadida kata ya Qash Wilaya ya
Babati mkoani Manyara.
Katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa watu kutoka pembe zote
za Wilaya ya Babati na nje ya Wilaya hiyo, hakuna kiongozi wa serikali wa
ngazi ya Wilaya na Mkoa aliyehudhuria mbali na viongozi wa vyama vya Siasa
akiwemo mbunge wa Babati vijijini Bw. Jitu Soni (CCM), Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wolaya ya Babati vijijini Bw. Nicodemus Tarimo huku
CHADEMA wakitumia wawakilishi.
Baadhi ya wanafamilia wa marehem Emiliana Kibuga wakihuzunika kwa kifo tata cha ndugu yao inayodaiwa kusababishwa na askari wa Tarangire |
Inadaiwa marehemu Emiliana alichukuliwa na timu hiyo Oktoba 16 asubuhi
ambapo jioni alirudishwa na askari hao akiwa taabani kwa ajili ya upekuzi
huku watoto wake Shaabani na Morgan wakiwa kwenye ulinzi mkali na kisha
kuondoka naye tena hadi walipopiqiwa simu na Polisi wakitakiwa kuchukua mwili
wa mtuhumiwa huyo.
mmoja wa watoto wa marehem Emiliana Kibuga akiuaga mwili wa mama yake mzazi |
Awali, kabla ya mazishi hayo pikipiki zaidi ya 200 na gari 70 za Kata hizo
zilisitisha kazi kwa ajili ya kwenda kuchukua na kuusindiki-mwili wa marehemu
toka mochwari ya hospitali ya Mrara mjini Babati hadi nyumbani, huku
wasindikizaji hao wakiwa na mapango yenye ujumla mbalimbali.
Baadhi tu yaliandikwa ' Lini mwanamke akauwa tembo? Paki (TANAPA) marufuku
kukanyaga Galapo na mwaka 2015 tembo waende kupiga kura'
huku wakilaani waliohusika na mauaji hayo.
Paroko wa Kanisa Katoliki Galapo Baba Eugene Kubasu akiongoza Ibada aliitaka
serikali kuhakikisha waliofanya unyama huo wanabainika na kuchukuliwa hatua za
kisheria na wao na wananchi kwa ujumla wapiga magoti wakimshitakia Mwenyezi
Mungu haki itendeke na si vinginevyo.
Mwakilishi wa Kamati ya mazishi Bw. Jumanne Mwanja akisoma wasifu wa marehemu
kwa niaba ya familia alisema kwa mujibu wa mume wa marehemu huyo Bw. Elias
Kibuga mke wake hakuwa na magonjwa ng'ang'anizi kama shinikizo la damu, sukari
au vidonda vya tumbo, amekuwa akiugua magonjwa yenye kutibika kwa urahisi.
Pia familia hiyo ilieleza kuwa kitendo kilichofanywa na timu ya Oporesheni
Tokomeza Ujangili dhidi ya mwanamke huyo na wengine nchini katika kipindi hicho
ni ukiukaji wa sheria za nchi hivyo kuiomba serikali kuchukua hatua wahusika
bila kuwaonea haya.
Mbunge wa jimbo hilo bwana Jitu akiweka shada la maua katika kaburi la Emiliana Kibuga anaedaiwa kuuawa na askari wa Tarangire |
Mbunge wa Babati vijijini Bw. Jitu alisema tukio hilo limewasikitisha sana kama
wabunge na kuahidi kwamba wabunge wote wa Mkoa wa Manyara watahakikisha sheria
inashika mkondo wake.
Hata hivyo licha ya umma kufurika kuuaga mwili huo huku wengi wao wakitamani
kushuhudia uso wa marehemu, familia ilikataa kata kata kuweka uso wazi kwa
madai ya sababu maalumu.
Add caption |
Wananchi kwa uapnde wao walilazimisha kufunguliwa kwa mwili huo, hadi Kiongozi
wa Kamati ya mazishi na musemaji wa familia Bw. Godwin Sanda alipowasihi
wananchi hao kukubaliana na uamuzi huo.
majirani, ndugu jamaa na marafiki wa familia ya Emiliana kibuga wakiuaga mwili wa mpendwa wao |
hatimaye mwili wa Emiliana umezikwa, NJUKI BLOG INAWAPA POLE WOTE WALIOGUSWA NA MSIBA HUO MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEM EMILIANA MAHALA PEMA PEPONI AMINA |