December 2013

KONDOA WILAYA KONGWE YENYE MIUNDO MBINU 'BUTU' NA MAISHA DUNI


Daraja hili halijawahi kupitisha gari kwa miaka kadhaa sasa, lakini limekuwa likijengwa karibu kila mwaka na kabomolewa na maji ya mbua...sijui kulikoni...na sijui fedha za ujenzi zinapatikana wapi! Daraja hili lipo kijiji cha Itiso barabara ya Kondoa-Bolisa.
Daraja la Kolo, Kondoa, hivi viongozi hawakuliona hilo miaka yote hiyo? Tushukuru Mwenyezi Mungu barabara hiyo sasa itajengwa kwa kiwango cha lami huenda ndio suluhisho la magari kupitia korongoni miaka yote  
Darasa la Kolo katika barabara ya Dodoma-Arusha, lilivunjika miaka zaidi ya 15 iliyopita hadi leo halijajengwa, lingekuwa na Sarenda Dar es salaam, Karanga Moshi au Nduruma Arusha ingekuweje?

WILAYA ya Kondoa mkoani Dodoma ni moja ya Wilaya kongwe nchini, inasadikiwa Iliana rasmi miaka 87 iliyopita, ikiwa ni miaka 35 kabla ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 na miaka 52 baada ya uhuru huo, yaani ilihali wa rasmi mwaka 1926.

Makao ya Makuu ya Wilaya hii inaaminika ndipo yalipokuwa Makao Makuu ya Jimbo la kanda ya Kati (Central Province) lilojumuisha Meiji mikuu ya Dodoma, Mpwapwa na Singida wakati huo,ambapo wakoloni wa Kijerumani wapokea kodi za mababu zetu mjini Kondoa pamoja na mikusanyiko na maamuzi yote ya utawala wa kikoloni ilifanyika hapo.

Jengo hili hapa chini linalosadikiwa kuwa iliojengwa mwaka 1902 na Wakoloni hao wa Kijerumani kwa nguvu za watanganyika wakati huo. Sasa jengo hilo linatumika kuwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kondoa na Ofisi zingine.




Wilaya hii licha ya ukongwe huo barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami ni kilomita tatu, tu kati ya tano zilizoahidiwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa safari zake Dkt. Jakaya Kikwete kati ya kilomita zaidi ya 800 za barabara wilayani hapa.

Lakini licha ya barabara ndefu na muhimu barani Afrika inayotoka Cape Town Afrika ya Kusini hadi Cairo Misri kupitia wilayani Kondoa na Chemba kwa zaidi ya kilomita 170 ndiyo kipande kilichobaki kirefu hakijajengwa kwa kiwango cha lami jambo linalokwamisha maendeleo ya wananchi wa eneo hili.
 

NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI SAMBAMBA NA UTORO DIDIMIZO LA ELIMU KITETO MKOANI MANYARA.



HALI ya maendeleo ya elimu wilaya ya Kiteto mkoani Manyara bado tete baada ya jamii kuendeleza kubariki ndoa za utotoni, mimba na utoro shuleni, huku siasa zikizidi kuathiri miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii kusita kuchangia maendeleo hayo.

Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA Bw. Samuel Kerinja akitoa neno la awali kabla ya Ufunguzi wa mkutano
                                           
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Kiteto na kushirikisha makundi mbalimbali wakiwemo, madiwani, Wenyeviti wa vijiji na watendaji, viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali na wawakilishi wa Halmashauri hiyo.

Hayo yalibainika juzi katika mkutano wa wadau wa maendeleo wakiwemo Madiwani, Wenyeviti wa Vijiji, Watendaji na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiseriali wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara kujadili taarifa ta utafiti wa maendeleo ya elimu na ujenzi uliofanywa na Shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Diwani kata ya Chapakazi  Lainumbe Mollel alisema wanachi wameathiriwa na siasa kwa kuwasilikiza zaidi wanasiasa badala ya kushughulikia shughuli za maendeleo, lakini pia kuchelewa kwa fedha kutoka serikali kuu ni sababu nyingine inayokwamisha mipango ya maendeleo siyo ya elimu tu bali ya Nyanja zote.
Alisema viongozi wa vitongoji na vijiji wamekuwa wakiitisha mikutano bila mafanikio wananchi hawataki kuitikia mikutano hiyo, sababu ni mipango ya maendeleo kuingiliwa na siasa, lakini pia wamekuwa wakipitisha bajeti Halmashauri za Wilaya lakini pesa hazifiki kwa wakati jambo linaloathiri mipango hiyo.
Diwani Viti maalumu   Zuhura Mavumbi alisema utafiti uliofanywa na KINNAPA umedhihirisha madhaifu makubwa katika maendeleo ya elimu wilayani Kiteto na kwamba hakuna budi kuhakikisha jamii inabadilika.
“Tafiti zinafanyika kweli lakini utafiti uliofanywa na KINNAPA umetuongezea ufahamu juu ya madhaifu tuliyonayo…watoto wetu sisi makabila ya Wanguu na Wamasai hatuna kazi nao zaidi ya kuwaozesha na kupokea mahari, maana yake ni kwamba bado Kiteto hatujapokea elimu ipasavyo kwani licha ya uhaba wa walimu na vifaa bado hali yetu ni mbaya” Alisema  Zuhura.




Afisa Miradi wa Shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA Bw. Dinno Celestian akiwasilisha mada katika mkutano huo wa wadau wa maendeleo ya Wilaya ya Kiteto

Awali Mratibu wa KINNAPA Samwel Kerinja alisema KINNAPA itaendelea kufanya tafiti na kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kijamii yanayoikabili jamii kwa jumla ili kusukuma maendeleo mbele hasa kwa jamii wafugaji na waokota matunda.
                                                      
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Nainge Lemalali akiugua mkutano wa wadau wa maendeleo wa Wilaya ya Kiteto mkoani



Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye pia ni Mwneyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Nainge Lemalali alisema hali ya Wilaya ya Kiteto kimaendeleo ni bora ukilinganisha na awali kwani imepiga hatua kubwa.
“Ni kweli hali ni mbaya lakini ukilinganisha na miaka 10 iliyopita bado tunaamini hatua kubwa tumepiga licha ya mapungufu kadhaa yaliyomo…jambo la muhimu ni kuhakikisha tunasonga mbele kwa kushirikiana na si kutupiana lawama bila kutafuta suluhisho kwa pamoja”Alisema  Lemalali.
Utafiti huo wa uwajibikaji ulifanywa na KINNAPA kwakushirikiana na Halmashauri ya Kiteto katika vijiji takribani 20 vya kata 13 kwa miaka miwili sasa wakiamini maendeleo huletwa na maarifa, ubunifu, mipango sahihi na bora, matumizi na usimamizi wa busara wa rasilimali zilizopo.


Mmoja wa wadau wa maendeleo wilayani Kiteto Bw. Fratern Kwahhison akichagia mada katika mkutano huo

M/KITI WA ZAMANI WA MONDULI DAVID PELLO AZIKWA NYUMBANI KWAKE MAKUYUNI, WAZIRI MKUU MSTAAFU BW. EDWARD LOWASSA AMWAGIA SIFA TELE TELE.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli na Diwani wa Makuyuni marehemu David Pello
                                                          
safari ya mwisho ya David Pello
                                                                           
 WAZIRI Mkuu Mstaafu Bw. Edward Lowassa amemwagia sifa aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Marehemu David Pello katika mazishi yake yaliyofanyika nyumbanai kwake Makuyuni leo.

Amesema anamjua Pello kwa mambo makuu matatu, kwanza alimsaidia sana mwaka 1993 katika maandalizi ya kugombea ubunge wa Monduli na hatimaye kunyakua  kiti hicho mwaka 1995, walipigana kufa kupona kuhakikisha kata ya Makuyuni haimegwi kwenda Mkoa wa Manyara wakati wa zoezi hilo miaka ya mwanzo ya 2000 lakini pia kuhakikisha Mji wa Makuyuni unapata maji ya uhakika.
                                                               
Mbunge wa Mondoli, Edward Lowasssa Akimsalimu mjane wa marehem
                                                          
WAZIRI Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho leo kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli na Diwani wa Makuyuni marehemu David Pello muda mfupi kabla ya mazishi yake nyumbani kwake Makuyuni, wilayani Monduli, Arusha.


"Nilipata habari nikiwa Mji wa Cape Town Afrika  ya Kusini mahali ambapo bahari za Atlantiki na Pasfiki zilipokutana nikalazimika kuondoka kuwahi kumzika ndugu yangu, ndugu yetu, lakini nasikitika kutokana na sababu zisizozuilika mke  wangu ameshindwa kufika...kubwa tuige mazuri ya David alikuwa binadamu kama sisi na hakosi makosa"Alisema kwa msisitizo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Bw. Vicent Parseko akitoa salamu alimtaja Pello kama mpiganaji mahiri katika maisha ya binadamu na kamwe hatosahaulika kwa juhudi zake katika kupigania maisha ya watu wa Makuyuni, Monduli na taifa kwa ujumla.

Mchungaji aliyeongoza mazishi hayo, Elijah Mollel alisema kifo cha Pello si huzuni kwa ndugu zake tu bali ni huzuni kwa wanadamu wote, na iwapo familia ilikuwa na mgawanyiko sasa ndio wakati wa kushirikiana pamoja kwani maisha yataendelea licha ya kutokwa na ndugu yao.

"Huu ni wakati wa mapambano baina yenu, ni wakati wa kupendana, kushikamana, kupambana kimaisha....hakuna sababu ya kuogopa kwani yatima mjane na watu wa Mungu, misiope kwani Mungu yupo na anaendelea kuwepo" alisisitiza.

Marehemu Pello alishirikilia kiti cha Udiwani kata ya Makuyuni kwa vipindi vinne na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli kwa vipindi viwili, Alizaliwa mwaka 1955  pia alikuwa Mwenyekiti wa viongozi wa Mila ya Kimasai (Laigwanani) kata ya Makuyuni hadi kifo chake. Alifariki ghafla Desemba 22 mwaka huu nyumbani kwake makuyuni.
                                                                  


Katika mazishi ya marehemu David Pello wa Makuyuni, katikati ni waziri Mstaafu na mbunge wa Monduli Edward Lowassa, kulia kwake Mwenyekiti CCM Wilya ya Monduli Reuben Kunei na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Bw.  Kasunga, kushoto kwake Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jaji Rutta na Mkuu wa Mkoa wa Singida Parseko Ole Kone
                                                      
Mh, Lowassa Akitoa neno la mwisho
                                                    
mh, Lowassa Akiaga kuondoka 
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya n

Newer Posts Older Posts