WANAFUNZI 48 WA SHULE YA KIISLAM YA CHAMANZI WAHITIM MAFUNZO YA SKAUTI
baadhi ya skauti wakitoka katika uchunguzi wa shughuli za kijamii katika tasisi mbalimbali kama polisi , sokoni, n.k, kama sehem ya mafunzo yao |
skauti wakisikiliza maelezo ya mkufunzi wao baada ya kutoka katika shughuli za kijamii |
Na Said Njuki Dar es Salaam
SKAUTI 48 wa Shule ya Msingi ya Kiislamu ya Chamazi wamepata
mafunzo ya kijasiri kwa lengo la kuwajenga kikakamavu ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya kujitegemea kimaisha.
"Malengo hasa ni
kumwandaa vijana w awe wakakamavu, jasiri waweze kujitegemea na hatimaye wawe ni msaada kwa
jamii ikiwa ni pamoja na kujiandaa kiakili kiutafiti kwa faida ya yake, na
taifa". Alisema Alhaj Omari Mavura Kamisha Msaidizi Skauti Makao Makuu.
Mavura alisema hiyo ni kambi ya Kwanza ya aina yake, ambapo
wasichana 27 na wa vulana 21 na ilikuwa
ya siku nne ambapo vijana hao wenye umri kati ya miaka saba na 12
waliweza kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulinzi wa maeneo yao.
Naye mkufunzi wa mafunzo hayo Bw. Mustafa Musoma alisema kwa
kawaida mafunzo hayo hufanyika mara nne
kwa mwaka ambapo mwezi wa Desemba mwaka
huu yatafanyika tena ili kwenda sambamba na mtazamo wa Shule wa kuwaandaa
vijana kikakamavu.
Mkuu wa Shule hiyo Bw. Abdallah Ngorini alisema viongozi wa
Shule hiyo hufarijika sana hasa vijana wanapofnya mazoezi kama hayo ni kujiweka
vizuri kiafya na kiakili.
Wakufunzi wengine ni Dotto Mohamed na Abdulrahim Nassoro wa
Markaz Gongolamboto.
tunakunywa chai baada ya kutoka katika mafunzo na shughuli hizo.
|