Na Janeth Raphael -Dodoma
CRDB Banki kupitia jina la Rais DK Samia Suluhu Hassan,katika hati fungane wamefanikiwa kukusanya zaidi ya sh bilioni 300 kwa ajili ya kuboresha miundombinu mbalimbali ya barabara.
Hayo yalibainishwa na Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Boma Lamara wakati akiwasilisha mada katika ufunguzi wa mkutano wa 39 wa ALAT unaoendelea katika ukumbi wa Jakaya Kikwete uliopo jijini Dodoma.
Lamara alisema fedha hizo zinakwenda kuwagusa moja kwa moja wakandarasi kutoka wakala wa barabara nchini TARULA ambao ni sehemu ya utekelezaji wa miundombinu ya Barbara.
Alisema wanajivunia sana kuwa CRDB kutokana na kuwa na ushirikiano mzuri na serikali katika utekelezaji wa mambo mbalimbali ya maendeleo hapa nchini,huku akisisitiza kuwa wataendelea kupiga hatua katika hilo.
"Tunajivunia kuwa CRDB kutokana na kuwa na mafanikio mengi katika mambo ya Maendeleo ikiwemo biashara na utoaji mikopo,"alisema Lamara.
Hata hivyo alisema CRDB wamekuwa ni wadau wakubwa wa ushiriki wa kikao kazi cha ALAT hiyo yote ni kutokana na kuwa na mahusiano mazuri na wadau wao ambao ni TAMISEMI ambapo alisema suala hilo linawafanya wajione wao NI Benki kiongozi.
Mbali na hao,pia benki hiyo imekuwa ikijihusisha na wakusanya pesa kwa ajili ya serikali kupitia mfumo wa GBG lakini pia wamejiunga na mifumo ya MUSE na TAUSI ili kujihakikishia kuwa mapato na matumizi yanafanyika vizuri.
Ukiacha hilo pia,wameanza kuwepo katika mchakato unaohusisha utoaji mikopo ya asilimia 10 Kwa makundi maalum na Kwa kufanya hivyo,wameanza kuwafikia wadau katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Kutokana na hilo,siku ya leo wamekusanyika
pamoja na watu kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo CRDB kutoa shukrani kwa Rais Samia kutokana na kuiamini benki hiyo kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali.

Tags
HABARI