viongozi wabainishwa kuwa chanzo cha migogoro ya wakulima na wafugaji
Na Said Njuki
WAKATI
migogoro ya wakulima na wafugaji ikishika kasi nchini, Mashirika yasiyo ya
kiserikali (NGO's) mkoani Manyara
yamedai kukithiri kwa migogoro hiyo kunatokana
na udhaifu wa uongozi bora na uwajibikaji kwa viongozi wa serikali.
Mashirika
hayo yamedai kitendo cha migogoro hiyo kuibuka kila kona ya nchi ni aibu katika
nchi inayotawaliwa kwa misingi ya utawala bora wakati viongozi wa serikali wa
ngazi mbalimbali wapo kila kona, lakini kila taarifa za migogoro hiyo zimekuwa
zikiripotiwa kila siku jambo ambalo ni hatari.
"Inasikitisha
kusikia migogoro ya wafugaji na wakulima karibu kila kona ya nchi yetu,wakati
viongozi wapo...matukio hayo ambayo mengine yanaambatana na mauaji huku wengine
wakijeruhiwa na kubakia na vilema vya maisha ni vielelezo wazi kuwa upo udhaifu
mkubwa wa utawala bora na uwajibikaji kwa viongozi wetu". Alisema Mratibu wa mtandao wa mashirika hayo Mkoa wa
Manayara (MACSNET) Bw. Nemence Mabung'ai.
Bw.
Mabung'ai alisema hayo katika mafunzo ya siku mbili ya wanachama wa mtandao huo
juu ya jinsi ya mbinu za kuandika historia za miradi yenye mafanikio
yaliyofanyiji mjini Babati Manyara na kuhudhuriwa na viongozi wa mashirika hayo
zaidi ya 30 kutoka Wilaya za Babati, Kiteto, Simanjiro, Hanang na Mbulu.
"
Serikali ya Tanzania ilishagawa kila eneo linamilikiwa na serikali za vijiji,
Wilaya, Mkoa na taifa na kila eneo
linalo viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa
...hata hivyo bado maeneo mengi yenye viongozi wa
serikali kuanzia ngazi ya Kitongoji, kijiji, kata, Wilaya hadi Mkoa sheria,za
ardhi zipo, lakini bado mapigano mengi
yanatokea kwanini kama siyo
uongozi mbovu na usiowajibika? " Alihoji Bw. Mabung'ai.
Alisema kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wamekuwa wakipambana na hali hiyo kwa muda
mrefu kwa kutoa elimu na kwamba kinachokwamisha kwa kiasi kikubwa ni viongozi
hao kutowajibika ipasavyo na kwamba mifumo ya uongozi na uwajibikaji
ingetekelezwa vizuri migogoro hiyo ingefikia mwisho.
Alishauri
viongozi wenye maeneo yenye migogoro hiyo wakae pamoja na wadau husika kupanga
kuweka mipango ya matumizi bora ya ardhi na kusimamia mipaka hiyo, tofauti na
hilo migogoro haitaosha nchii.
Kiongozi wa
Shirika lisilo la kiserikali la Hanang
Wemen Concelling Development Association
(HAOCODA) Bi. Rose Tippe alisema tatizo ni utendaji mbovu kwa wasimamizi wa
sheria, lakini bado mashirika hao yanafanya kazi kubwa ya na yanastahiki
pongezi kwa jitihada zao katika kupigania haki za wafugaji na wakulima hao