mahafali ya 5 ya shule ya sekondary Chamanzi




 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro (MUM) Bw. Issa Omari Malichela akitoa hotuba katika maafali ya tano ya Chamazi Islamic Seminary Jumapili 20/10/2013. Bw. Malichela ndiye alikuwa mgeni rasmi katika maafali hiyo
.

Na Said Njuki Dar es Salaam

MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro (MUM) Bw. Bilali Majuva amewataka Walimu wa Shule nchini kubuni njia mbadala za kusomesha wanafunzi  na kuacha kuwabebesha lawama wanafunzi hao kuwa  hawasomesheki.
wanafunzi wakisoma risala

Amesema kila mtoto anao uwezo wa kuelewa atakachosomeshwa na Mwalimu wake ipasavyo, bali baadhi ya walimu wamekuwa wakiwatuhumu wanafunzi kuwa hawasomesheki jambo ambalo si kweli.
"Hakuna mwanafunzi asiyefundishika duniani, yapo malalamiko toka kwa baadhi ya walimu kuwa baadhi ya wanafunzi hawasomesheni jambo ambalo si kweli...huko ni kukwepa majukumu...wazazi wamewaletea watoto, wakawaamini mnaweza kuwapa elimu na maadili mema, hawataki tena kusikia wanafunzi hawasomesheki, fundisheni watoto wanaweza acheni kuwabebesha lawama" Alisema Bw. Majuva.

Wahitimu wavulana wa Shule ya Sekondari ya Chamazi Islamic Schools katika maafali ya 5 ya Shule hiyo yaiyofanyika Jumapili Oktoba 20 mwaka huu shuleni hapo.
 
waliohitim, wasichana nao wapo
Bw. Majuva alitoka rai hiyo Jumapili hii katika maafali ya 5 ya kidato cha IV ya Shule ya Sekondari ya Chamazi Islamic Seminary yaliyofanyika shuleni hapo ambapo wanafunzi zaidi ya 40 walihitimu.
Akizugumza katika maafali hayo mgeni rasmi Bw. Issa Omari 'Malicela' ambaye pia ni Mahadhiri katika Chuo hicho aliitaka Jamii kuelewa kuwa elimu ndiyo msingi wa maendelo yoyote duniani.
Alisema kitendo cha kudharau elimu yoyote ni kichocheo cha kazama katika lindi la umaskini duniani, hivyo kukwamisha jitihada za serikali na wadau wa maendeleo katika mapambano dhidi ya umaskini.


Mwenyekiti wa Bodi ya Chamazi Islamic Centre (CIC) Dk. Hadi Mruke akitoa neno kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro Issa Omari 'Malicela' (aliyeketi kulia kwake) katika maafali ya tano ya Shule ya Chamazi Islamic Seminary yaliyofanyika juzi shuleni hapo ambapo wahitamu 40 walikabidhiwa vyeti vyao. (Picha kwa Hisani ya Njuki Blog).

Awali Mkuu wa Shule hiyo Bw. Yusuf Kokole alitoa changamoto kadhaa zinazoikabili Shule ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maabara kwa ajili ya masons ya Kemia, Fizikia na baiolojia, maktaba, Bwalo kwa ajili ya chakula, msikiti na kubainisha kuwa tatizo kubwa ni uwezo mdogo wa kiuchumi.
Shule ya chamazi Islamic seminary ipo kijiji cha Chamazi Mbagala wilayani Temeke Dar es Salaam inayo wanafunzi kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha VI ni mekuwa ikfanya vizuri.

Kikundi cha Skauti cha Chamazi Islamic Islamic Schools kikifanya mambo yake Jumapili Oktoba 20 mwaka huu katika maafali ya 5 ya IV Mwaka huu



baadhi ya wageni waalikwa


Newer Post Older Post

Leave a Reply